LuvTouch Zanzibar Coconut Soap
LuvTouch Zanzibar Coconut Soap
Regular price
$3.50
Regular price
Sale price
$3.50
Unit price
/
per
Share
Sabuni ya LuvTouch Zanzibar Coconut Soap imetengenezwa kwa kutumia mafuta ya nazi asilia (Virgin Coconut Oil - VCO). Sabuni hii imesheheni ndani yake mafuta ya nazi ya asili ambayo yana utajiri wa protini na ni nzuri kwa ngozi nyeti (sensitive), yaliyotengenezwa na mafuta ya nazi fresh yasiyopikwa au kuchemshwa. Ndani yake pia yamechanganywa kwa asilimia kidogo mafuta ya Alizeti na mafuta ya Mise yote kukupa Vitamin E, SPF 15 na Vitamin K. Vitamin E huimarisha ngozi na kuondoa wrinkles, SPF hulinda ngozi kwa mionzi ya jua na Vitamin K husaidia kukazisha ngozi na pia husaidia kupunguza michirizi (stretch marks). Sabuni hii hutoa povu zuri na kwa urahisi hata katika maji ya chumvi. Pia inatakatisha sana, utaona utakapoitumia inaondoa uchafu, jasho na mafuta kwenye ngozi yako kwa haraka. Kwa kifupi, inafanya kazi ya usafi kwa upole, lakini kwa uhakika mzuri hasa kwa ngozi yako ya usoni.
Sabuni ya LuvToch Zanzibar Coconut Soap imetengenezwa maalum kwa kila aina ya ngozi na ina upole wa kutosha kwa ngozi nyeti. Sabuni ya LuvTouch Zanzibar Coconut Soap ina uhodari wa kuilinda na kuilainisha ngozi yako kuwa soft hasa kwa wanawake na vijana – inaweza kutumika kama sabuni ya uso, kuogea mwili mzima au kwa kunyolea ndevu kwa wanaume. Made in Zanzibar!