SOYA MILK POWDER
SOYA MILK POWDER
Preço normal
$6.00
Preço normal
Preço promocional
$6.00
Preço unitário
/
por
Share
23/12/2020
GEEDASA ENTERPRISES
Apr 02, 2019
AFYA: Faida Za Kunywa Maziwa Soya
Na Dokt Gerly Daniel Sandor
gerldaniel43@gmail.com
MAZIWA SOYA hutupatia angalau vitamini zote kama vitamini A, D, E na hadi K. Pia yana madini ya calcium.
*Hujenga na kulainisha ngozi*
Vitamini na virutubisho vilivyomo ndani ya maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora.
Huimarisha meno
Maziwa soya ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu yaani Calcium. Pia huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D.
Huimarisha mifupa
Watoto wanahitaji kunywa maziwa soya ili kuimarisha ukuaji wao. Pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa soya ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa au kitaalamu Osteoporosis. Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D.
*Kujenga misuli*
Maziwa soya yanachangia katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana kwenye maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi. Hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena. Maziwa soya huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali.
*Kupunguza uzani*
Wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa soya wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda. Pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula chakula (appetiser).
*Huzuia maumivu wakati wa hedhi*
Wanawake wengi hupata maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamethibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.
*Huongeza nguvu mwilini*
Je, unaishiwa nguvu mapema au kuchoka sana? Unahitaji virutubisho vilivyomo kwenye maziwa. Hivi vitaupa mwili wako nguvu mpya na kukufanya kuwa mwenye nguvu siku nzima.
*Huondoa kiungulia*
Kiungulia husababishwa na asidi zipatikanazo tumboni. Hivyo maziwa soya (ambayo si mgando) hutengeneza utando maalumu tumboni ambao hupambana na asidi hizi.
Kwa hiyo unywaji wa maziwa soya (ambayo si mgando) utakusaidia kupambana na tatizo la kiungulia.
*Hupambana na maradhi mengine*
Utafiti umebaini kuwa maziwa huzuia magonjwa. Magonjwa au hali hizi ni kama vile shinikizo la damu. Inaaminika pia maziwa soya hupunguza lehemu (cholesterol) saratani n.k