Skip to product information
1 of 4

LuvTouch Zanzibar Manjano Sabuni

LuvTouch Zanzibar Manjano Sabuni

Regular price $ 3.50
Regular price Sale price $ 3.50
Sale Sold out
Tax included.
Kichwa

Sabuni ya LuvTouch Zanzibar Manjano imeungwa na unga asilia wa Manjano (Turmeric) na inafaa sana kwanza aina zote. Sabuni ya Zanzibar Manjano hukinga ngozi yako na bakteria zinazosababisha kupatwa na chunusi na pia kusaidia kuondoa madoa yaliyoachwa na chunusi. Kwa karne na karne, mabibi na mama zetu walikuwa wakitumia unga wa Manjano wakichanganya na maji kidogo na kuweka kwenye ngozi matatizo ya ngozi zao hasa chunusi. Pia unga wa Manjano mpaka hivi leo hutumika katika kumsinga bi harusi mtarajiwa ili kupata ngozi nyororo na yenye mvuto siku chache kabla ya kuolewa.

Sabuni ya Zanzibar Manjano imetengenezwa maalum kwa kila aina ya ngozi na ina upole wa kutosha kwa ngozi nyeti. Sabuni ya LuvTouch Zanzibar Manjano ina uhodari wa kuilinda na kuilainisha ngozi yako kuwa laini hasa kwa wanawake na vijana – inaweza kuonekana kama sabuni ya uso, kuogea mwili mzima au kunyolea ndevu kwa wanaume. Imetengenezwa Zanzibar!

View full details